The House of Favourite Newspapers

Diamond Adai Sekta ya Muziki Haina Shukrani, Atoa Tamko Zito Kuhusu Rayvanny

0
Diamond Platnumz

SUPASTAA wa Bongo Fleva na CEO wa Lebo ya WCB, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameamua kuvunja ukimya na kuanika kile anachokiona kufuatia sakata la wasanii wake anaowasaidia kuwanyanyua katika lebo yake wakishapata umaarufu wanamkimbia na kuanzisha vita ya kibiashara na yeye.

 

Kupita kwenye comment aliyoiandika katika ujumbe uliochapishwa na kaka yake @romyjons ambaye pia ni official DJ wake, akimashauri lupambana na muziki wake zaidi kuliko kusaidia wasanii ambao baadaye wanaanza kumsema vibaya pembeni na kumkebehi, Diamond ameandika;

 

“Hivi saa ndio nimegundua kwanini watu kama kina Kidayo (Wizkid), Davido na kadharika waliamua kufocus na nafasi zao na sio kupoteza nguvu, umaarufu, pesa na muda wao kusaidia wasanii chipukizi walowa-sign.

 

“Hii industry haina shukrani! But usiumie hii ni nchi yetu na ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunaendelea kunyanyua vijana toka mtaani ili nao wajikomboe kimaisha,” amesema Diamond.

Diamond Platnumz amesema tasnia ya muziki haina shukrani

Ikumbukwe kuwa kauli hii inakuja ikiwa ni takribani miezi miwili tangu aliyekuwa msanii wake, Rayvanny kuondoka katika lebo hiyo huku wasanii hao wakifikishana Basata ili kufikia maafikiano ya kumalizana kwa amani.

 

Mbali na Vannyboy, wasanii wengine waliowahi kuondoka WCB ni Harmonize na Rich Mavoko. Wasanii anaowasimamia kwa sasa Diamond katika lebo yake ni Zuchu, Lavalava, Mbosso na Queen Darleen ambaye hata hivyo ni kama amesimama kufanya kazi za muziki.

Leave A Reply