The House of Favourite Newspapers

Diamond Agawa Chakula kwa Wakazi wa Tandale – Pichaz + Video

STAA wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platinumz’ amewakumbuka wakazi wa Tandale kwa kuwagawia chakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Idd El Fitri.

Diamond ametoa msaada huo leo Ijumaa, Juni 15, 2018 ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka wakazi wa tandale ambako ndipo haswa alikozaliwa na kukulia, kuanza muziki kabla ya kuwa staa.

Imekuwa utamaduni wa msanii huyu mkubwa Tanzania na Afrika nzima kuwasaidia watu wenye kipato cha chini hasa kwenye sikukuu kwa kuwapa vyakula ili nao washerehekee vyema sikukuu hizo na familia zao.

Diamond ametoa msaada wa mchele (kilo tano kila mtu), nyama (kilo mbili kila mtu) na pesa taslim kiasi cha Tsh. 5,000/= kwa kila mkazi wa Tandale aliyefika nyumbani kwao na Diamond ambapo tukio hilo lilikuwa likifanyika.

Comments are closed.