The House of Favourite Newspapers

Misri ya Mo Salah Wapigwa na Uruguay ya Suarez – Video

TIMU ya Taifa ya Misri imeshindwa kufurukuta mbele ya Uruguay baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0, mechi yao ya kwanza katika michuano ya Fainali ya Kombe la Dunia 2018 zinazoendelea nchini Urusi.

 

 

Katika game hiyo, Misri walijitahidi kwa kiasi kikubwa kuzuia mashambulizi ya Uruguay huku wakishambuliana kwa zamu hali iliyopelekea hadi wanakwenda mapumziko walikuwa sare ya bila kufungana.

Mchezaji wa Barcelona na Uruguay, Luis Suarez alikosa mabao kadhaa langoni mwa Misri lakini bahati ilikuwa kwao kwani kunako dakika za lala salama, dakika ya 89 ya mchezo, Uruguay kupitia kwa Jose Gimenez, walipata bao la ushindi.

 

Licha ya Mo Salah kutajwa kuwa huenda angecheza baada ya afya yake kuimarika kutokana na kuumizwa bega na beki wa Madrid, Sergio Ramos kwenye fainali za UEFA, staa huyo wa Misri na Afrika hakuweza kucheza, badala yake alitazama mechi yote akiwa benchi.

 

Katika Kundi A, wenyeji Urusi wanaongoza wakiwa na pointi 3 na mabao 5 baada ya kuichapa Saudi Arabia jana, Uruguay anafuata akiwa na pointi 3 na bao 1,  wa tatu ni Misri na wa mwishoi nia Saudi Arabia.

 

Uruguay wameendelea kuweka rekodi yao ya kutokufungwa na Timu za Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia huku kipa wa Misri, Mohamed El-Shenawy akiondoka kama mchezaji Bora wa mechi ‘Man of the Match’ kwa kuokoa michomo mingi ya Uruguay.

Highlights FIFA World Cup 2018: Egypt vs Uruguay

Comments are closed.