The House of Favourite Newspapers

Diamond Avunja Rekodi ya Mwaka Australia

diamondKAMA ilivyo kawaida yake kutotoka vinywani mwa mashabiki, mkali wa Afro-Pop Diamond Platnumz ame-make headline, hii ya leo sio Bongo ni nchini Australia.
Siku moja baada ya DW kuitaja ngoma aliyoshirikishwa na marehemu Papa Wemba, Chacun Pour Soi kuwa imefunga mwaka kwa kuwa namba moja katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Kidogo aliyowashirikisha P-Square nayo imefunga mwaka kwa kishindo.
Wimbo huo umekuwa wimbo wa mwaka katika kituo cha redio cha Radio Afro cha Australia, baada ya kuzishinda nyimbo za magwiji wengi wa Afrika wakiwemo Wizkid, Davido, Tiwa Savage na wengine kibao.
Diamond ameshukuru kwa nafasi hiyo kwa kusema, “Thank you AUSTRALIA thank you RADIO AFRO…. KIDOGO ft P -SQUARE Song of the Year #RADIOAFRO.”

Diamond Platnumz ft P’square KIDOGO (Official Video)

Comments are closed.