The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kufungiwa Damond, Rayvanny Waiangukia Serikali – (VIDEO)

 

BAADA ya wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny kukiuka masharti ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kufanyia shoo wimbo wa ‘Mwanza Nyegezi’ uliofungiwa na baraza hilo , hatimaye wawili hao wameomba radhi kwa kufanya hivyo.

 

Wameweka video katika akaunti zao za Instagram huku Diamond akinukuliwa akiomba radhi: “Habari, naitwa Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz na mwenzangu Raymond Shabani Mwakyusa, maarufu kama Rayvanny.

“Kwa unyenyekevu mkubwa tunaomba radhi Jamhuri yetu Tukufu ya Tanzania, Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Baraza letu la Sanaa la Taifa (Basata) na kila aliyekwazika kwa kupafomu wimbo wa mwanza katika shoo yetu ya wasafi festival Mwanza.

 

“Japo tunajitahidi kuwa vijana wenye mfano bora katika taifa letu, lakini kama ujuavyo binadamu sikuzote hatuwezi kupatia na ikatokea siku tukakosea, na kweli tumekosea kwa kupafomu ule wimbo ambao umefunguwa“.

 

Lakini hakuishia hapo pia aliahidi kutorudia kosa hilo ambalo walilitenda yeye na mwenzake: “Tunaahidi kutorudia tena kwa kosa lililotokea lakini pia kupitia kazi zetu za sanaa kuwasihi mashabiki na wasanii wenzetu kuwa mabalozi wazuri  wa tamaduni zetu za Tanzania. Asante“.

Maelezo yanayoambatana na video hiyo yanasomeka: “Japo tunajitahidi kuwa vijana wa mfano bora kwenye Taifa letu, lakini kama tulivyoumbwa binadam hatuwezi kupatia siku zote, lazma itatokea siku tutateleza tu….Ila Utelezapo, ni vyema kulijua Kosa na Kulirekebisha ili kesho na Kesho kutwa lisijirudie….

Inshaallah Mwenyez Mungu Atusimamie na kutuongezea Juhudi na Maarifa katika Kazi zetu ili kwa Pamoja tuzidi kuukuza Muziki wetu na Kuendelea Kuiwakilisha vyema na kulipa sifa Nzuri na Heshima Nchi yetu….Tuseme Amin…..🙏🏻

 

BASATA iliahidi kuwachukulia hatua wasanii hao baada ya kukiuka masharti na kudharau kauli ya baraza hilo kwa kufanyia shoo wimbo huo. Mpaka wakati huu hakuna jibu lolote kutoka BASATA kuhusiana na maobi hayo ya msamaha.

 

TAZAMA WAKIOMBA RADHI HAPA

 

Comments are closed.