The House of Favourite Newspapers

DIANA AJIGANDISHA KWA WEMA

Diana Kimari

BAADA ya kudaiwa kuwa msanii wa Bongo Muvi, Diana Kimari ni kati ya marafiki wa Wema Sepetu waliotakiwa kuwa mbali naye, mrembo huyo amefunguka kuwa, yeye bado anampenda Wema na hakuna wa kuwatenganisha.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Diana alidai kuwa hakuwahi kutetereshwa na maneno ya waja, akasisitiza; ‘wanaodhani na mimi nimewekwa mbali na Wema na ndiyo maana simposti kwenye ukurasa wangu wa Insta kama ilivyokuwa huko nyuma, wanachekesha’.

 

“Niwafahamishe tu kwamba hakuna wa kunitenganisha na Wema, yule ni rafiki, ni kama dada yangu, tumegandana, manenomaneno sitaki, waniache na maisha yangu,” alisema Diana.

STORI: Imelda Mtema

DIAMOND ATUA SUMBAWANGA KWA NDEGE, MAPOKEZI YAKE BALAA! (VIDEO)

                  PART 1

 

                 PART 2

Comments are closed.