The House of Favourite Newspapers

UKARIBU NA WEMA, DIANA KIMARI ATOA YA MOYONI

Diana Kimari

BAADA ya kunangwa na mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamii kisa kuwa karibu na mrembo Wema Sepetu, msanii wa filamu Bongo, Diana Kimari ameamua kutoa ya moyoni kuwa acha waendelee kumnanga lakini hawajui maisha yake halisi.  

 

Mashabiki wengi walikuwa wakimuona msanii huyo kuwa kitendo cha kufuatana na Wema kitamfanya awe mtu wa kujichanganya viwanja kwa sababu ameokoka.

Akizungumza na Ijumaa, Diana alisema kuwa watu wengi kwenye mitandao ya kijamii hawajui kabisa maisha halisi ya mtu zaidi ya kukisia na kumsema vyovyote wawezavyo ndio maana hawafuatilii.

 

“Unajua ni hivi wamenisema sana hapa katikati lakini hawajui kamwe maisha yangu na uzuri najitambua havinisumbui kabisa najua nini nataka maishani mwangu kwa hiyo hata kama wakinitukana ni sawa kwa vile siwalipii bando,” alisema Diana. Diana amekuwa na ukaribu na Wema kwa kipindi sasa ambapo ukaribu huo umemfanya hadi kujichora tattoo yenye jina la Wema.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.