The House of Favourite Newspapers

Diddy Amtetea Mkuu wa Revolt Dhidi ya Ubaguzi wa Rangi

MWANAMUZIKI Puffy Diddy wa Marekani amemtetea mkuu wake wa mtandao wa televisheni wa Revolt, Roma Khanna, dhidi ya madai ya ubaguzi wa rangi katika kampuni hiyo.

Amefanya hivyo kutokana na barua iliyotumwa kwa kampuni hiyo kutoka kwa mfanyakazi wa zamani akidai mkuu huyo alikuwa anafanya vitendo vya ubaguzi kazini.

Mfanyakazi huyo alidai kwamba Khanna alikuwa amepunguza asilimia 30 ya wafanyakazi wa Revolt, na asilimia 99 yao walikuwa Wamarekani wenye asili ya Afrika.

Roma Khanna.

Diddy amekanusha madai hayo akisema kampuni hiyo inayomilikiwa na watu weusi haina na haivumilii vitendo vya ubaguzi wa rangi,  na hivyo Khanna ataendelea kuwa mkuu wa kampuni hiyo.

“Asilimia 67 ya watu wa kampuni yetu ni wa mataifa mbalimbali na zaidi ya asilimia 60 ya uongozi ni wanawake.   Hivyo madai kwamba kuna ubaguzi dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika, ni ya kipuuuzi na yanaudhi,” alisema Diddy.

Comments are closed.