Dilunga na Kagere Wanawaumiza Watu Huko..

JKT Tanzania imejichimbia visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi na mchezo wao wa kwanza dhidi ya Simba Agosti 23 na akili zao zipo kwenye safu ya kiungo ya Wekundu hao. Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Mohamed Abdallah ‘Bares’ alisema;

 

“Tupo sehemu tulivu, mafunzo yanakaa kwenye vichwa vya wachezaji kwa umakini mkubwa. “Kila mchezaji ana morali kubwa na matarajio yetu kurejea Bara itakuwa Agosti 20, mashabiki watupe sapoti kwani tunajua mchezo wetu dhidi ya Simba utakuwa mgumu ila tupo tayari,” alisema na kuongeza kwamba wataiduwaza Simba.

 

Msimu uliopita wa mwaka 2018/19 JKT Tanzania iliacha pointi sita kwa Simba na ilifungwa jumla ya mabao matatu ambapo kwenye mchezo wa kwanza mfungaji alikuwa ni Meddie Kagere aliyefunga mabao yote mawili na mchezo wa pili mfungaji alikuwa Hassan Dilunga.

Loading...

Toa comment