Dimpoz meno nje filamu mpya ya JB

ommy (1)Ommy Dimpoz.

MKALI wa Bongo Fleva anayetarajia kuachia ngoma yake mpya ya Achia Body Leo, Ommy Dimpoz amejikuta akivunjika mbavu kwa jinsi alivyoona mwigizaji Jacob Steven ‘JB’ alivyouvaa uhusika wa kuigiza maisha ya Nasibu Abdul ‘Diamond’ katika filamu yake mpya, Chungu cha Tatu.

Ommy alisema sinema hiyo ambayo imetoka mapema wiki hii, JB na Wema wamefunika vibaya kiasi ambacho kila akiitizama anakauka kwa kicheko maana wameuvaa uhusika wa namna ambavyo Wema amekuwa akiumizwa na penzi la Diamond walipokuwa wapenzi.
“Ni bonge la filamu aisee,” alisema Dimpoz.


Loading...

Toa comment