The House of Favourite Newspapers

DINNO: NILIPANGA KUMTUMIA MASOGANGE KWENYE VIDEO YANGU

Kufuatia kifo cha video vixen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’, msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetesa na ngoma yake mpya ya Bado Upo, Abdallah Manyuti ‘Dinno’ amefunguka kwamba alipanga kumtumia mwanadada huyo kwenye video ya wimbo huo lakini Mungu akamchukua kabla malengo yake hayajatimia.

 

“Kifo cha Masogange ni pigo kubwa sana kwangu kwa sababu kwanza alikuwa ni dada yangu ambaye tunaheshimiana kwa muda mrefu, mimi na yeye tulijuana miaka mingi iliyopita kwenye kazi zangu hizi za sanaa.

“Sasa baada ya kuachia audio ya wimbo wangu, menejiment yangu ya Nambiza Entertainment ilipendekeza tumtumie Masogange kama video queen, wazo ambalo hata mimi nilikuwa nalo siku nyingi,” alisema Dinno na kuongeza kwamba baada ya makubaliano hayo, alimtafuta Masogange kwa njia ya simu na kuzungumza naye lakini akamwambia kwamba kwa sasa amesitisha kwa muda kufanya kazi.

“Aliniambia nisubiri kidogo atanipa majibu lakini kabla hajanipa majibu ndiyo likatokea la kutokea, moyo unaniuma sana kwa kweli, Mungu ampumzishe kwa amani,” alisema Dinno kwa masikitiko.

Comments are closed.