The House of Favourite Newspapers

DIVA ALIA: Watanzania Nisaidieni Nizae, Nishakata Tamaa – Video

MTANGAZAJI maarufu, Diva The Bawse ameweka wazi kuwa anahitaji mchango wa kiasi cha dola $7,000 (sawa na Tsh. Milioni 15) kwa ajili ya matibabu ya kutungishwa mimba kwa mfumo wa kisasa wa IVF (In Vitro Fertilisation) nchini Marekani, hii ni baada ya kuambiwa na madaktari kuwa hataweza kutunga mimba kwa njia ya kawaida.

 

Diva akieleza kwa hisia kali amesema kuwa mwezi uliopita alienda Hospitali ya TMJ kufanya vipimo na aliambiwa kuwa mirija yake ya uzazi ina hitilafu (blockage) hivyo hawezi kutunga mimba kwa njia ya kawaida mpaka kwa mfumo wa kisasa wa kupandikiza mbegu wa IVF Treatment.

 

Diva amewaomba Watanzania wamchangie kiasi cha pesa kupitia akaunti yake ya Benki na akaunti ya GoFundMe ili aweze kufanikisha tiba hiyo.

VIDEO: MSIKIE DIVA AKIFUNGUKA

Comments are closed.