The House of Favourite Newspapers

Diva Asitisha Michango ya Ujauzito

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ baada ya kuomba mchango wa shilingi milioni 15 kwa ajili ya kwenda kusaka mtoto nje ya nchi, amesitisha zoezi hilo na kudai kuwa sasa yupo tayari na wakati ukifika atakwenda kwani ameamua kulifanya suala hilo kuwa lake na ameshapata pesa.

 

 

Diva alisema kuwa, anamshukuru Mungu amepata pesa na wakati ukifika atakwenda kufanyiwa huduma ya kupandikizwa ujauzito ili atimize ndoto yake ya kuitwa mama.

 

“Nilisitisha kuchukua michango, nimeamua suala hilo liwe la kwangu. Hivyo, nina bajeti yangu mwenyewe nimeihifadhi kwa ajili hiyo. Nasubiri wakati muafaka ufike, naamini nami nitaitwa mama,” alisema Diva.

STORI: Hamida Hassan.

Comments are closed.