visa

Lulu Diva ana nguo hadi anasahau

MWANAMUZIKI Lulu Abbas ‘Lulu Dava’ ameibuka na kusema kuwa linapokuja suala la kuvaa kwake hana mchezo kwani ana chumba kizima kwa ajili ya nguo na viatu tu ambapo inafikia wakati hata hakumbuki amerudia nguo lini.  Akizungumza na Amani, Lulu alisema kuwa pamoja na maendeleo anayoyafanya katika maisha yake lakini suala la mavazi humchukulia sehemu kubwa ya pesa zake kwani ana viatu vingi na nguo ambazo hata wakati mwingine hakumbuki kuzivaa.

“Kiukweli ninajipenda sana  linapokuja suala la kuvaa na kuonekana mrembo natumia pesa kwani nina viatu vingi ukiacha raba ambazo nazo zina idadi yake na nguo ndio usiseme,” alisema Lulu.

Aidha, Lulu alishangaza zaidi aliposisitiza kuwa ana chumba maalumu kwa ajili ya ishu ya mavazi tu wakati wengine chumba kinakuwa kimejaa kila kitu na kulala humohumo. “Kutokana na wingi wa mavazi yangu nimekitenga chumba kwa ajili ya mavazi tu, humo utakuta kila aina ya nguo na aina ya viatu pamoja na Dressing Table ya kujifanyia make up,” alisema Lulu Diva.
Toa comment