The House of Favourite Newspapers

Diwani Aliyetuhumiwa Kufukia Kisima cha Maji Buchosha Ajisalimisha kwa Shigongo

0

Diwani wa Kata ya Irenza, Mneke Mauna aliyekuwa akituhumiwa na wananchi kwa madai ya kufukia kisima walichopewa fedha za kukichimba na na mbunge wa jimbo hilo, Eric Shigongo hatimaye amejisalimisha kwa mbunge huyo na kutaka wafanye kazi pamoja na kusahau yaliyopita.

Tukio hilo limejitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Shigongo uliofanyika katika Kijiji cha Irenza ambapo amemwomba mbunge huyo waendelee kushirikiana kuwaletea wananchi maendeleo.

“Tusahau yaliyopita, tunapaswa kusonga mbele tuwatumikie wananchi wetu waliotuchagua na tuweke tofauti zetu pembeni,” amesema Mneke kwenye mkutano huo.

Machi 27, 2023 wananchi wa Kitongoji cha Nyangalamila B waliandamana wakimtuhumu diwani huyo kufukia kisima hicho, hali iliyoleta taharuki kubwa.

Baada ya kisima hicho kufukiwa, Shingongo alifanya jitihada nyingine kuwasaidia wananchi wa kitongoji hicho kupata kisima kingine kitakachowasaidia kupata maji safi na salama.

Kupitia Wizara ya Maji, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini wilayani Sangerema (Ruwasa), walichimba kisima kirefu cha maji kwenye kitongoji hicho chenye thamani ya Sh. milioni 42 ambacho tayari kinatoa huduma ya maji kwa wananchi.

Kwa upande wake, Shigongo amewaambia wananchi kuwa tofauti zao zimeisha hivyo amewaomba kuwaunga mkono ili kutekeleza Ilani ya CCM kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa Kata ya Irenza na wakazi wa Buchosa kwa jumla.

Leave A Reply