The House of Favourite Newspapers

Dj wa Kike Anayewachezesha Wazungu Atua Global Radio – Video

Dj wa kike Mtanzania anayeishi nchini Ujerumani, Lydia Philly ‘Deejay Aisher’.

INASEMEKANA kawaida kuwa kile mwanaume anaweza kufanya, mwanamke pia anaweza kufanya tena ikawa vizuri zaidi. Kuna mwanamke Mkenya anayeamini katika hili hadi kufikia kiwango cha kuingia katika uwanja unaotawaliwa na wanaume kwenye tasnia ya burudani.

Deejay Aisher akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Bongo255 ‘Lady Mufasa’ kutoka +255 Global Radio

Lydia Philly alimaarufu kama Deejay Aisher ni mzaliwa kutoka Migori, nchini Kenya; Ambaye kwasasa anafanya shughuli zake za u’ DJ nchini Ujerumani.  Jina la Deejay Aisher limekuwa likikua na kujizolea umaarufu zaidi kutokana na aina ya muziki ambao amekuwa akiucheza kama DJ .

…Akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Bongo255, Stewart George, wa +255 Global Radio

“Niliamua kuwa DJ kwa sababu ya shauku na mapenzi yangu kwenye muziki,” Deejay Aisher alisema katika mahojiano aliyofanya ndani ya kipindi cha Bongo255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio.

Aliendelea kwa kusema, “Nimekuwa tofauti na DJ’s wengi wa kule kwa sababu ya aina ya muziki ambao nimekuwa nikicheza, kuna muziki ukisikika kwa kule Ujerumani wanajua ni mimi kutokana na ustadi na mbinu niwapo kwenye deki.”

…Akiwa kwenye deki akionyesha ufundi wa ku-mix ngoma.

Kwa mujibu wake, “DJ mzuri ni yule anayeweza kuchanganya muziki vizuri bila kuvuruga. DJ mzuri pia ana uwezo wa kuchanganya muziki wa aina tofauti na kuwafanya watu waburudike.”

Tangu aanze kuishi nchini Ujerumani toka mwaka 2011 ambapo alienda kwa ajili ya masomo, Aisher amekuwa akijali zaidi  kuupromoti na kuucheza muziki wa Kiafrika nchini Ujerumani.

…Akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Bongo255,  ‘Juju Dafa’,  wa +255 Global Radio

Mwaka huu pekee Aisher ameshinda tuzo tatu ikiwamo ya Diaspora Night Awards, Tuzo ya DJ Bora wa Mwaka, na DJ Bora Ujerumani. Pia amewahi kushiriki jukwaa moja kufanya back up ya muziki kama DJ wa wasanii kadhaa wa Afrika, wakiwamo Mr Flavour, Timaya, Kizz Daniel, J Martins, Sauti Sol, Eddie Kenzo, Maleya, Burna Boy  na Diamond Platnumz

Comments are closed.