The House of Favourite Newspapers

Dk Shika Alivyopata Shavu La Sokabet (Video)

0
Dk Louis Shika.

MSOMI na ‘bilionea’ aliyejipatia umaarufu hivi karibuni baada ya kutaka kununua nyumba za mnada za mfanyabiashara, Said Lugumi, Dk Louis Shika amepata shavu lililosababisha gumzo kuanzia jana Jumapili.

 

Jumapili ya jana ikiwa tulivu maeneo mengi, ghafla katika mitandao ya kijamii kukaanza kusambaa video fupi ikimuonyesha Dk Shika akiitangaza Kampuni ya Sokabet ya nchini Tanzania ambayo inajihusisha na mauala ya michezo ya kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali.

 

Video hiyo ilianza kusambaa majira ya saa nne asubuhi ya jana, lakini ndani ya saa chache, mitandao karibu yote ya kijamii kulikuwa na video ya tangazao hilo ambapo kuanzia WhatsApp, Instagram, YouTube na Facebook kote Shika alikuwa hashikiki.

Ilikuwa kama kichekesho lakini asilimia kubwa ya waliotoa maoni waliipongeza Kampuni ya Sokabet kwa kutumia fursa ya umaarufu wa mtu huyo kutangaza biashara yao lakini pamoja na kumuongezea kipato mzee huyo ambaye msemo wake wa 900 Itapendeza umekuwa kama wimbo wa taifa.

 

Gazeti la Championi Jumatatu likaamua kumtafuta Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda ambaye alitoa ushirikiano mzuri kwa kufafanua kile kilichotokea.

 

“Kwa kweli wazo la kumtumia Dk Shika awali lilionekana kama siyo sahihi lakini ndani ya muda mfupi kampuni yetu ikaona ni kitu kizuri na ingefaa atumike ili kuendeleza uzalendo wa kujali vitu vya vyumbani.

 

“Kama unavyojua Sokabet ambavyo imekuwa ikitengeneza mazingira ya kujali vitu vya nyumbani Tanzania, mfano udhamini wetu kwa timu ya Majimaji inayoshiriki Ligi Kuu ya Bara, tuliona ni kitu kizuri tumpe neema mzee wetu hiyo.

“Tulimtafuta na tukamweleza wazo letu, akatukubalia na akatutajia kiasi ambacho angependa tumatie, baad aya mazungumzo tukakubaliana kumpatia kiasi ambacho amekitaka, na tukapanga muda kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kutengeneza tangazo hilo.

“Huwezi kuamini tulisema tufanya mazoezi lakini Dokta ni mwelewa sana, maneno tuliyokuwa tukimwelekeza kuyaongea wakati wa tangazo na vitendo alifanya kwa urahisi sana.

 

“Tukiwa studio hatukupata naye tabu kutengeneza tangazo hilo, tulimaliza ndani ya muda mfupi, baadaye tukaelekea Uwanja wa Karume kwa ajili ya kurekodi vipande akiuchezea mpira.

 

Pawasa amfundisha soka Dk Shika

“Huko ndipo kazi ilipokuwa kubwa (anacheka), unajua yule ni mtu mzima na siyo mtu wa mazoezi, hivyo suala la kuuchezea mpira lilikuwa gumu kwake, lakini tukiwa pale, tulipata nafasi ya kukutana na beki wa zamani wa Taifa Stars na Simba, Boniface Pawasa ambaye aliamua kuja kutupa maelekezo ya kitu fulani.

 

“Pawasa alitusaidia mbinu fulani za kuuchezea mpira na kumpa maelekezo Dk Shika.

“Tunaamini ulikuwa uamuzi mzuri na tumepanga kuendelea kushirikiana na Dk katika masuala mengine kadhaa.

 

“Lengo ni kuwapa ajira Watanzania ili kuboresha hali ya uchumi kama ambavyo kumekuwa na mamilioni ya wananchi wanashiriki kwenye kubet matokeo kupitia tovuti yetu ya www.sokabet.com,” alisema Franco.

 

Kuhusu masuala ya soka, Shika aliliambia gazeti hili kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Chelsea ya England.

 

Mastaa waipokea vizuri

Muda mfupi baada ya video hiyo kutoka, baadhi ya watu maarufu walioiweka kwenye kurasa zao za kijamii ni Mange Kimambi, Soud Brown wa Clouds FM ambaye alisema anatamani Dk Shika angekuwa baba yake kisha yeye angekuwa ndiye mhasibu wa mzazi wake huyo.

Stori: John Joseph | Championi Jumatatu

Leave A Reply