The House of Favourite Newspapers

Dk. Tulia achaguliwa kuwa Naibu Spika kwa 71.2%

0

dk tulia (1)

Dk. Tulia Ackson Mwansasu akila kiapo mara baada ya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge.

dk tulia (2)

Dk. Tulia Ackson Mwansasu wakati akiomba kura kwa wabunge.

sakaya

Magdalena Sakaya akiomba kura kwa wabunge.

Aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson Mwansasu hivi punde amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata jumla ya kura 250 sawa na 71.2% huku mpinzani wake Magdalena Sakaya (CUF) akipata kura 101 sawa na 28.8%.

Dk. Tulia hivi karibuni aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kuwa mbunge baada ya kutenguliwa uteuzi wake kama Naibu Mwanasheria Mkuu.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Tulia alikuwa akiwania nafasi ya Uspika wa bunge  baada ya kuteuliwa na  Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini yeye na mgombea mwenzake Abdullah Ali Mwinyi walijitoa na kumuachia Job Ndugai awanie nafasi hiyo.

Leave A Reply