The House of Favourite Newspapers

Dkt. Abbasi Awaunganisha Nature (TMK) na GK (East Coast)

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali leo amewasisitiza wasanii wa Tanzania kuwa, pamoja na kazi zao mbalimbali, wanawajibu na jukumu moja kubwa zaidi la kuibrand na kuitangaza nchi yetu Tanzania bila kuendekeza tofauti zao.

 

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo aliposhiriki kipindi cha XXL kinachorushwa na Radio Clouds FM leo Disemba 22, 2020, Dar es Salaam, kilichowakutanisha meza moja kwa mara ya kwanza wasanii wakongwe na waasisi wa makundi katika muziki wa kizazi kipya, Gwamaka Kaihula aka King Crazy GK kutoka East Coast Team na Juma Nature aka Sir Nature kutoka TMK Wanaume.

Wasanii hao ambao watashiriki Tamasha Kubwa la Muziki la Serengeti (Serengeti Music Festival) linaloandaliwa na Wizara ya Habari na kufanyika Disemba 26 Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, ni sehemu ya wasanii wa muziki na wadau wengine wa sanaa kama Bongo Movie, maigizo na sanaa nyingine zaidi ya 70, watakaoshiriki katika Tamasha hilo kubwa na la aina yake nchini.

 

“Nimeweta hapa kuonesha kuwa nchi yetu bado inaheshimu uasisi wao wa Bongofleva na bado wanamchango hata sasa. Hawa GK na Nature ni mfano wa wasanii ambao wanabrand zao lakini mwisho wa siku wanasimama pia kuitetea na kuitangaza brand moja kubwa ambayo ni nchi yetu Tanzania,”alisema Dr. Abbasi akisisitiza kuwa Wizara hiyo sasa inakwenda kuimarisha zaidi muunganiko wa sanaa na utalii katika kuitangaza nchi yetu.

Leave A Reply