The House of Favourite Newspapers

Dkt. Kikwete Kuongoza Harambee ya Kukusanya Futari Kwa Ajili ya Yatima

0


Taasisi isyo ya kiserikali ya VOLUNTEERS IN DEVELOPMENT imeandaa harambee ya kuchangisha futari kwa ajili ya YATIMA waishio majumbani kwao na familia zao.

 

‘’Tumeamua kuunganisha nguvu zetu kuwafikia Yatima na wasiojiweza waishio majumbani kwa kuwa wana changamoto za mahitaji Zaidi ukilinganisha na wale wanaoishi kwenye vituo maalum. Tuna jumla ya familia 286 zenye Zaidi ya yatima 850 kwenye mikoa mbali mbali bara na visiwani ambayo ni Dar es salaam, Bagamoyo, Mkuranga, Tanga, Arusha, Mwanza na Pemba ’’ amesema Bi. Tune Shaaban Salim, mwenyekiti wa taasisi hiyo.

Mahitaji ya chakula kwa kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni pamoja na, tambi, sukari, tende, maharage, unga wa ngano, unga wa sembe/dona, mafuta ya kupikia, mchele na pamoja na nguo za sikukuu. Kiasi kisichopungua Tsh 54,611,000 kinahitajika ili kuweza kukidhi mahitaji kwa idadi ya watoto hao

KUHUSU HARAMBEE
Shughuli hiyo itafanyika siku ya jumamosi Tarehe 10 April 2021 kuanzia saa 1:00 jioni katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam. Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ndio atakayekuwa mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo akifuatana na viongozi wengine wa serikali, viongozi wa kidini, pamoja na wafanya biashara mbalimbali

KUHUSU VID.

Volunteers In Development (VID) ni Jumuiya ya Wanawake iliyosajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali (NGO) yenye makao yake makuu Magomeni, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Taasisi ilianza huduma hizi za kijamii mwaka 2011na kuilisajiriwa rasmi mwezi wa April mwaka 2014 chini ya sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 Ikiwa na namba ya usajili 00NGO 00007127.

MAFANIKIO
Kwa takriban miaka kumi sasa tumekuwa tunawapatia huduma ya chakula kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani (futari), nguo za sikukuu na vifaa vya elimu watoto walioandikishwa kwenye tassisi yetu. Tumekuwa tukilifanikisha hili kwa kutumia ichango ya wanachama, ndugu, jamaa, marafiki , wadau mbalimbali wa maendeleo ya jamii washio ndani na nje ya nchi, ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania, pamoja na akampuni ya Brooklyn Media, Mohammed Enterprises na ASAS Mpaka sasa kwa upande wa Elimu, taasisi inamudu kusaidia kuwahudumia mahitaji watoto 645 tu ambao wanasoma katika shule za serikali za sekondari na msingi.

 

Miongoni mwao wapo watoto wenye magonjwa andamizi wapataothalathini na tisa (39) magonjwa hayo ni pamoja na kisukari, seli nundu, pumu na hata waishio na virusi vya HIV ambao inawalazimu kuwa na bima za afya kukidhi mahitaji yao ya Matibabu mara
kwa mara wauguapo.

Taasisi hii pia imefanikiwa kuwapeleka vijana 13 (wa kike na wa kiume) kupata mafunzo ya ufundi stadi – VETA, baadhi yao wanaendelea na masomo na wengine wameshapata ajira na wamekuwa msaada mkubwa kwa familia zao.

Mbali na Yatima, vile vile tunasaidia wagonjwa wenye hali ngumu za kimaisha wanaposhikwa na maradhi yenye kuhitaji gharama kubwa za matbabu na upasuaji. Tayari tumeshasaidia wagonjwa thelathini na mbili (32) toka tuanze shughuli hizi za kijamii.

‘’VID ina lengo la kuanzisha kituo cha mafunzo (Training Centre) VID COMMUNITY CENTRE ili kufundisha kazi za ujasiriamali kwa yatima, wasiojiweza, wahitaji na wajane. Hatua ya kwanza katika hili ni kununua eneo ambalo tayari tumefanikiwa kulipia
na kununua jingo kwenye Plot No 388, Block AA eneo la Makumila, Mburahati, Manispaa ya Ubungo. Tunategemea Center hiyo itakua chanzo cha mapato endelevu baadae, ili kupanua zaidi wigo wa huduma zetu kwa jamii’’. Amesema Bi. Zubeda Shomary Said, meneja miradi wa taasisi hiyo

 

‘’Kutokana na ongezeko la Yatima, tumepata changamoto ya kukidhi mahitaji yao kikamilifu na kwa wakati husika , hivyo basi tunayaomba mashirika binafsi, taasisi mbalimbali, watu binafsi, wafanyabiashara na jamii kwa ujumla wajitokeze kushirikiana
nasi katika kulikamilisha jukumu hili. Jukumu la kulea yatima ni la jamii kwa ujumla, tunaomba ushirikiano wenu kwa hali na mali’’. alisema Bi Khadija Sheikh msemaji mkuu wa taasisi.

Leave A Reply