The House of Favourite Newspapers

Dkt. Msonde: Tehama Kuboresha Elimu Nchini

0
Naibu  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  anayeshughulikia  Elimu, Dkt. Charles Msonde amesema Serikali imetoa vifaa vya TEHAMA  kupitia Mradi wa  Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (Boost) ili kuboresha mafunzo  endelevu ya walimu  kazini na  wanafunzi kujifunza.
Akizungumza leo kwenye uzinduzi wa  ugawaji wa vifaa vya TEHAMA kwa vituo vya walimu  (TRC)  wa shule za Msingi na Awali jijini Dodoma vilivyogharimu Sh.Bilioni 6.9, Dkt.Msonde amesema kuwa walimu watakuwa na uwezo wa kufundisha kupitia mtandao kwa kutumia TEHAMA jambo ambalo litasaidia kuboresha elimu nchini.
“Vifaa hivi vitawawezesha wanafunzi  kusoma na mwalimu mmoja anaweza kufundisha somo moja kwa wanafunxi wa shule mbalimbali kwa kutumia TEHAMA, hii itasaidia hasa maeneo yenye upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi kuweza kufundisha kwa shule ambayo haina mwalimu   kupitia TEHAMA,” amesema  Dkt.Msonde
Amesema kuwa ni malengo ya Serikali katika kuhakikisha inaboresha elimu  kwa kuboresha elimu kwa kujenga miundombinu bora na  kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Leave A Reply