The House of Favourite Newspapers

Dkt Reginald Mengi, Shigongo Watoa Heshma zao za Mwisho Kuuaga Mwili wa Ruge Mutahaba

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, akipita mbele kutoa heshma zake za mwisho.

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Group, Eric Shigongo ni miongoni mwa waombolezaji waliotoa heshma zao za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba ambaye ameagwa leo jijini Dar es Salaam tayari kuelekea nyumbani kwao Bukoba kwa ajili ya pumziko lake la milele.

Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Group, Eric Shigongo (kulia) akipita mbele ya jeneza lenye mwili wa Ruge Mutahaba kutoa heshma zake za mwisho.

Viongozi hao walitoa heshma zao za mwisho leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo pia wakazi wa jiji hilo waliungana na wanafamilia katika kutoa heshma zao za mwisho.

Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye miwani) akimpa pole mmoja wa wafiwa.
Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (wa pili kushoto) akipita mbele ya jeneza lenye mwili wa Ruge Mutahaba kutoa heshma zake za mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Redio cha EFM na TVE, Francis Ciza maarufu kama DJ Majizzo na Elizabeth Michael wakiwa katika nyuso za huzuni msibani kwa Ruge kabla ya kutoa heshma zao za mwisho.
Mzazi mwenzake na marehemu Ruge Mutahaba, Zamaradi Mketema (katikati) akiwa katika nyuso za huzuni kabala ya kutoa heshma zake za mwisho kwa mpendwa wao.
Waombolezaji wakipita mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Ruge Mutahaba katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam wakitoa heshma zao za mwisho.
Waombolezaji wakiendelea kupita mbele ya jeneza kutoa heshma zao za mwisho.
Msanii wa Bongo Fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz (kushoto) na Msanii, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ wakihuzunika kumpoteza mpendwa wao.
Mwandishi wa habari wa Global Publishers, Imelda Mtema (mwenye kilemba kichwani) akimfariji Zamaradi Mketema ambaye ni mzazi mwenzake na marehemu Ruge Mutahaba.
Zamaradi Mketema akitoa heshma za mwisho.
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) akitoa salamu za pole kwa wafiwa.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL

Comments are closed.