The House of Favourite Newspapers

Dkt. Tulia: Milioni 50 Kila Kijiji Haipo, Rais Samia Hakuahidi

0


Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amewataka wabunge kutombebesha Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan mzigo ambao hastahili kwamba hakuahidi kutoa TZS milioni 50 kila kijiji.

 

Dkt. Tulia amesema hayo bungeni mjini Dodoma na kueleza kuwa katika kampeni zake za uchaguzi wa mwaka 2015, Rais Samia, ambaye wakati huo alikuwa mgombea mwenza hakutoa ahadi hiyo.

 

“Waheshimiwa wabunge tusianze kumtwika Rais wetu mambo ambayo hajaahidi ikiwa ni pamoja na hili la milioni 50,” amesema kiongozi huyo.

Leave A Reply