The House of Favourite Newspapers

DNA Ya Tiffah….

0

12132803_1635458573371970_728412592_n1
Musa Mateja na Issa Mnally,

Dar es Salaam: Taarifa njema kwa Giant wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwanaye Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ kuwa hivi karibuni walipima vinasaba vya damu (DNA) na kujihakikishia kuwa mtoto huyo ni damu yake, imeibua makubwa.

AMANI LA KWANZA KURIPOTI
Habari hiyo iliyoibua gumzo kwenye mitandao ya kijamii Afrika Mashariki na Nigeria iliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti ndugu la hili, Amani la wiki iliyopita baada ya kupewa ‘ubuyu’ huo kisha kufanya mahojiano maalum na Diamond aliyeeleza kuwa vipimo hivyo alivifanyia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ akiwa na mama mtoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Diamond-Tifah-1qaDiamond alikaririwa: “Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali nikachoka, nikawa njia panda. Ili kuondoa figisufigisu, nikamwambia Zari twende nikapime DNA na Tifah kabla sijaanza ziara ya Marekani.”
Diamond alieleza kuwa vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa Tiffah ni mtoto wake na siyo mtoto wa Ivan Ssemwanga ambaye ni mume wa zamani wa Zari aliyeishi naye kwa takriban miaka kumi.

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI
Baada ya habari hiyo kuwaingia mashabiki wake ndipo yakaibuka madai kutoka upande wa pili nchini Uganda ambapo ilielezwa kuwa rafiki wa Ivan, King Lawrence ndiye aliyeanza kupinga vipimo hivyo na kwamba, Zari alimuingiza mkenge Sauz.

Hata hivyo, habari hiyo imeendelea kushikiwa bango na mitandao ya Uganda inayodai kuwa Zari ni mjanja na ndiyo maana aliamua vipimo hivyo vikafanyikie Sauz kwa kumtumia daktari wake.
Kwa mujibu wa akina King Lawrence, wao wanataka Diamond aache kushikwa masikio na badala yake atafute vipimo halisi bila kumhusisha Zari au daktari wake.

FB_IMG_1452056101471MADAI YAUNGWA MKONO NA DAKTARI BONGO
Madai hayo yaliungwa mkono na daktari maarufu jijini Dar, Dokta Kalunde wa Dispensary ya Vijana, Kinondoni, aliyezungumzia ishu hiyo akimlalamikia Diamond kuwa kwa nini akapime DNA nchini Afrika Kusini wakati vipimo hivyo vinapatikana Bongo?

“Kwanza ametengeneza picha mbaya kuwa labda Tanzania hakuna vipimo vya DNA wakati vipo na watu wanapima na kupata majibu yao vizuri, tena kila siku.
“Unajua inawezekana kabisa huyo Zari akawa alimseti daktari wake kwa hiyo nashauri waje wapime hapahapa Bongo na waandishi washuhudie au waone majibu halisi. Hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza ubishi,” alisema daktari huyo akiomba kuhifadhiwa jina.

PEDESHEE KATUNZI VIPI?
Hata hivyo, gazeti hili lilipomtafuta pedeshee maarufu Bongo, Muzamir Issa Katunzi ambaye naye aliwahi kuhusishwa na Tiffah ili kujua anachukuliaje majibu hayo ya DNA alisema kwa kifupi kuwa kwa sasa hataki malumbano na Diamond.
“Kwanza siwezi kubishana na mtoto mdogo kama Diamond, kama ni watoto mbona ninao wengi? Sitaki kabisa malumbano na huyo Diamond,” alisema Pedeshee Katunzi kisha akakata simu.

ZARI (2)TUMRUDIE DIAMOND
Gazeti hili lilipomtafuta Diamond ili kujua anachukuliaje madai hayo ya wapinzani wake juu ya vipimo hivyo wanaodai kuwa ‘ameshikwa masikio’, aliendelea kusisitiza kuwa Tiffah ni damu yake na ameshajihakikishia kwa vipimo.

“Sijawahi kupigiwa simu nyingi kuhusu habari kama nilizopokea kipindi hiki. Ndiyo hivyo wengine wananipongeza lakini wengine wananilalamikia kuwa mbona sijawashirikisha. Mimi nawajibu tu kuwa mambo mengine siyo lazima kila mtu ajue.

“Pia ndicho kipindi ambacho nimepokea simu nyingi za interview za redioni, tivii na kwenye magazeti. Mimi ninachokisema ni kwamba Tiffah ni mwanangu na nina uhakika,” alisema Diamond.

Leave A Reply