The House of Favourite Newspapers

Dogo Janja Afunguka Video Yake Kufanana na ya Diamond

0

MSANII Dogo Janja amesema kuwa hawezi kulalamika kwa video ya wimbo wa  Nuru kufanana location na ule wa Diamond,  uitwao Jeje.

 

Video za nyimbo hizo ambazo zimefanyika visiwani Zanzibar zinaonekana kufanana baadhi ya location kitu kilichoibua maswali nani kaiga kwa mwenzake lakini video ya Diamond ndiyo ilitangulia kutoka.

 

 Dogo Janja amesema kilichotokea hawezi kukilalamikia kwani kosa si lao bali waongozaji wa video hizo. “Siwezi kulalamika, siwezi kuwa na malalamishi, muziki wangu ni mkubwa sana sidhani kama natakiwa niwe na malalamishi madogo-madogo.

 

“Pia hii nadhani ni kosa wa waongozaji kwa sababu kuna pesa ikilipa wewe unaenda kushuti tu video, unakuta kila kitu kipo tayari, kwa hiyo package yangu ilikuwa haihusiani na location,” amesema.

 

Wimbo wa Dogo Janja uliongozwa na Hanscana na ile ya Dimaond iliongozwa na Kenny ambaye amekuwa akifanya video za msanii huyo na wengine wa WCB.

 

Leave A Reply