The House of Favourite Newspapers

Dogo Janja: Albamu Hapana! Bado Naangalia Upepo

0

fab5dogo2Bjanja2Bmy2Blife

Na Leonard Msigwa

Mwanamuziki Abdulaziz Abubakari ‘Dogo Janja’ anayetamba kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva na nyimbo za My life na mpya aliyotoa siku za hivi karibuni iitwayo Kidebe ameweka wazi hayuko tayari kutoa albamu mpya siku za hivi karibuni mpaka hapo soko la kuuza muziki kwa mfumo wa albamu nchini utakapo kaa sawa.

Akizungumza na Global Digital, Dogo Janja alifunguka kwa kusema, “Sipo tayari kutoa albamu mpya kwa sasa japokuwa lolote linaweza kutokea, bado menejimenti inaangalia upepo wa sokoni ulivyo, huwezi kutoa albamu kama hali ya sokoni ni mbaya.” Alisisitiza Dogo Janja.

Alipoulizwa zaidi mbali na muziki anajishughulisha na nini alisema, “Nafanya biashara ndogondogo tu kwani huwezi tegemea muziki pekee yake usawa huu maisha yalivyo magumu, lazima tuzisake hata nje ya muziki.” Japo hakuwa tayari kuweka wazi aina gani ya biashara anaifanya.

Leave A Reply