The House of Favourite Newspapers

Drake amvalisha Rihanna pete ya uchumba

0

rihanna-wearing-diamond-ring-during-the-billboard-music-awards-lead-2Mwanamuziki Robin Rihanna Fenty na rapa Aubrey Drake Graham ‘Drake’ wameingia kwenye vichwa vya habari mitandaoni baada ya Drake kumvalisha Rihanna pete ya uchumba ya almasi yenye thamani ya Dola Milioni 1.

Pete hiyo yenye uzito wa gramu 16 ilivaliwa na Rihanna kwenye Tuzo za Billboard, mazingira yaliyoonesha kuwa wawili hao siyo kwamba ‘wanadate’ tu bali ni wachumba.

rihanna-drakeDrake na Rihanna

Rihanna na Drake waliwahi kuwa wapenzi mwaka 2014 ambapo Drake alimfuata mdada huyo jijini London, nchini Uingereza ambako huko walionwa wakifanya mahaba chooni katika mgahawa mmoja maarufu.

rihanna-ring-miami-heat-game-may-8-lead-1Kipindi hicho Rihanna alivishwa pete yenye thamani ya Dola 42,000 lakini uchumba wao uliishia njiani kabla ya hivi karibuni kuamua kurudiana na kuingia kwenye hatua hiyo ya uchumba kuelekea kwenye ndoa.

Leave A Reply