The House of Favourite Newspapers

Droo ya pili ‘shinda nyumba’ yafaana!

0

1.MC-Chaku akimpigia simu mmoja wa washindi wa Bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba mbele ya wasomaji waliofika kushuhudia mchezo huo.MC-Chaku akimpigia simu mmoja wa washindi wa bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba mbele ya wasomaji waliofika kushuhudia droo hiyo ya pili.
2.Mhariri Kiongozi wa Magazeti pendwa ya Global, Osca Ndauka (kulia) akipiga simu ya mshindi baada ya kuchezeshwa droo na kutangazwa mshindi. Kushoto ni Mhariri Mtendaji,Richard Manyota.Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka (kulia) akimpigia simu ya mshindi baada ya kuchezeshwa droo na kutangazwa mshindi. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Global, Richard Manyota.
3.Kutoka kushoto ni Elvan Stambul,Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha , Bakari Majjid na Mhariri Mtendaji wa Globa,Richard Manyota.Kutoka kushoto ni mhariri mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli, mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Majjid na Mhariri Mtendaji wa Global, Richard Manyota wakifurahia burudani iliyokuwa ikiendelea viwanjani hapo.

nyumba (10)Majina ya washindi wa droo ya pili ya Shinda Nyumba iliyochezeshwa jioni ya leo eneo la Karume jijini Dar.
4.Kuponi zilivyoonekana za kutoka mikoa mbalimbali ya hapa nchini.Kuponi zilivyoonekana za kutoka mikoa mbalimbali nchini.
5.Mtoa burudani maarufu kwa jina la 'Toto Tundu'akifanya yake kabla ya droo hiyo kuchezeshwa.Mtoa burudani maarufu kwa jina la Toto Tundu akifanya yake kabla ya droo hiyo kuanza kuchezeshwa.
6.Kuponi zikimwagwa chini kwa ajili ya kuanza zoezi la kuchanganywa kuwapata washindi.Kuponi zikimwagwa chini kwa ajili ya kuanza zoezi la kuchanganywa na kisha kuwapata washindi.
7.Mmoja wa aliyefika kwenye bahati nasibu hiyo akichanganya kuponi ali kumtafuta mshindi.Mmoja wa wafuatiliaji wa droo hiyo ya pili akichanganya kuponi ili kumtafuta mshindi.
8.Zoezi likiendelea la kuchanganya kuponi. Zoezi likiendelea la kuchanganya kuponi.
9.Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi ,Elvan Stambul akizungumza jambo mara baada ya kumalizika droo hiyo ya bahati nasibu.Mhariri mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli akizungumza jambo mara baada ya kumalizika droo hiyo ya bahati nasibu.
10..Mc-Chaku akifanya mahojiano na baadhi ya wasomaji wa Magazeti ya Global juu ya mchezo huo wa bahati nasibu.MC-Chaku akifanya mahojiano na baadhi ya wasomaji wa Magazeti ya Global juu ya mchezo huo wa bahati nasibu.
11.Chaku akiendelea kufanya mahojiano kupitia Global TV ONLINE.MC-Chaku akiendelea kufanya mahojiano kupitia Global TV Online.
12.Mahojiano yakiendela baada ya kumalizika droo ya pili ya Shinda Nyumba.Mahojiano yakiendela baada ya kumalizika kwa droo ya pili ya Shinda Nyumba.
13Mmoja wa watu waliohudhuria kwenye droo hiyo ya pili akichanganya kuponi kabla ya kumtafuta mmoja wa washindi.
14Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza, Happiness Haule akichanganya kuponi ili kumpata mmoja wa washindi wa droo ya pili katika Viwanja vya Karume Dar.
15….Akiwa ameshaiokota kuponi ya mshindi kabla ya kutangazwa.

DROO ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers iliyofanyika jana maeneo ya Karume, Ilala jijini Dar na kushuhudiwa na wasomaji kadhaa wa magazeti ya kampuni hiyo ilifaana baada ya washindi wa zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki, kupatikana.

Droo hiyo ni ya pili baada ya ile ya awali iliyofanyika Januari saba mwaka huu katika Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar. Katika droo kubwa mshindi wa kwanza atajinyakulia zawadi ya nyumba ya kisasa iliyopo maeneo ya Salasala Dar.

Kabla ya kufanyika kwa droo kubwa hapo jana ilitanguliwa na droo ya papo kwa hapo ambapo Adam Richard na Chezary Mbuko walijishindia kofia huku Shaban Mneke akiondoka na fulana.
Katika droo ndogo ya pili, Halima Bashemela wa Igunga, Tabora alijishindia shuka na Francisco J. Kilalo wa Tandika, Dar alijinyakulia vyombo vya chakula (dinner set).

Washindi wa Ving’amuzi vya Ting walikuwa ni Agnes Pallangyo wa Singida, Samwel Sailot na Thomas Kilala wote kutoka Arusha, Robert Wilson na Ramla Mussa wakiwa ni wakazi wa Dar.
Emmanuel Henry wa Toangoma, Dar alijishindia Smartphone, huku Mshindi wa Pikipiki ya Skymark akiwa ni Lucy M. Swai wa Kibaha, Pwani.

Akihutubia umati uliokusanyika katika droo hiyo Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli aliwataka wananchi kujaza kuponi zinazopatikana katika magazeti ya Global Publishers ambayo ni Uwazi, Championi, Risasi Jumatano, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani, Risasi Jumamosi na Ijumaa.

“Mshindi wa nyumba anaweza kuwa wewe, niwaombe wananchi wote mnunue magazeti hayo ambayo yanatoka kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi. Shilingi yako mia tano inaweza kukufanya umiliki nyumba ya kisasa kabisa, huwezi kuamini lakini jaribu mshindi anaweza kuwa wewe,” alisema Stambuli.

Naye Mwakilishi wa Kig’amuzi cha TING, Simon Make alisema wameamua kushirikiana na Global katika promosheni hiyo na akasema wanatoa ving’amuzi hivyo bora kwa wasomaji wa magazeti hayo ili wawe mabalozi wa kuuthibitishia umma ubora wake.

(HABARI/PICHA: DENIS MTIMA NA RICHARD BUKOS/GPL)

Leave A Reply