The House of Favourite Newspapers

Droo ya Pili ya Baba Lao, Washindi 6 Wajazwa Mkwanja

0
Shabiki wa Simba Sc, Humphrey Msungu akichukua moja ya kuponi zilizochanganywa ili kumpata mshindi. Kushoto Mkuu wa Idara ya Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam na kulia ni mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Elibariki Sengasenga wakishuhudia zoezi hilo.

DROO ya pili ya bahati nasibu ya Jishindie Gari na Championi na Spoti Xtra (maarufu kama promosheni ya Baba Lao ama Chomoka na Gari Mpya Toyota Fun Cargo) ilifanyika leo Jumanne, Aprili 21, 2020 katika ofisi za Global Group na kufanikiwa kupata washindi sita.

 

Hii inakuwa ni idadi kubwa ya washindi ukilinganisha na ile droo ya kwanza ambayo ilitoa washindi watatu kutoka katika mikoa tofauti. Washindi wote sita ambao wametoka katika mikoa mbalimbali watazawadia fedha taslimu shilingi 50,000 kila mmoja pamoja na tisheti mpya.

Shabiki wa Simba Sc, Humphrey Msungu akichanganya kuponi hizo kabla ya kuchagua kuponi moja ya mshindi.

Droo hiyo ambayo imechezeshwa na shabiki wa Simba Sc, Humphrey Msungu, imerushwa na Televisheni namba moja ya mtandaoni nchini, Global TV Online, ili kuweka wazi kwa washiriki wengine na Watanzania wote kwa ujumla na kuondoa ile dhana ya kwamba washindi huenda wanatengenezwa.

Anthony akimpigia simu mshindi.

Mkuu wa Idara ya Masoko wa Global Publishers ambao ndiyo waandaaji wa promosheni hiyo kupitia magazeti yetu ya michezo, Championi na Spoti Xtra, Antony Adam aliwataja washindi hao kuwa ni Yassin Seleman wa Kibaha Pwani, Samson Kabuje wa Mbeya, Aloyce Mdolwa wa Mwanza, Hassan Khatau wa Dar es salaam, Mwinjuma Ngayama wa Tanga na Yuda Mrema wa Moshi.

Adam alitoa sababu ya kubadilisha zawadi ya  kutoa simu katika droo ya kwanza na kutoa fedha, akisema kuwa ni kujali hali za wananchi kutokana na janga la Corona ambapo watu wengi hawana fedha za kujikimu kutokana uchumi kuyumba.

“Tumeamua kubadilisha zawadi kidogo safari hii kutokana na ishu ya Corona, watu wengi ni kama hawana fedha kutokana na uchumi kutokuwa sawa kutokana na Corona, kwahiyo tukitoa shilingi 50,000, itawawasaidia katika kununua mahitaji mbalimbali ya nyumbani katika kipindi hiki.

Mtangazaji wa Global TV Online na +255 Global Radio, Lukas Masungwa akizungumza na mshindi wa droo ya pili.

“Kwahiyo kila mshindi atatumiwa fedha yake kesho Jumatano, ambapo mbali na fedha tutawapatia pia na zawadi za tisheti kama nyongeza,” alisema Anthony.

 

Bahati nasibu hii, itatoa zawadi ya gari mpya ana ya Toyota FunCargo, hicho ndiyo kitu pekee ambacho unatakiwa kukizingatia, hizi simu na zawadi nyingine kama fedha na tisheti ambazo zitakuwa zinatoka kwenye droo ndogo kabla ya ile kubwa kufanyika mwezi ujao. Jaribu kurusha karata yako ya kiume sasa, kwa kusoma gazeti la Championi kwa shilingi 800 tu, kila wiki na Spoti Xtra kwa Tsh 500 tu.

 

Anthony akizungumza na wanahabari kuhusu droo hiyo na zawadi watakazopatiwa washindi hao sita.

JINSI YA KUSHIRIKI

Nunua Gazeti la Championi, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

 

JINSI YA KUTUMA:

Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.

 

Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Elibariki Sengasenga akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa droo hiyo.

MASHARTI YA KUSHIRIKI:

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

 

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

WASHINDI SITA WA BABA LAO WATOKA NA 50,000/= | SHINDANO A SPOTI XTRA NA CHAMPIONI

Leave A Reply