The House of Favourite Newspapers

Duma: Johari ananikuna sana

MSANII wa filamu Bongo Muvi, Daud Michael ‘Duma’, amesema kuwa anakunwa na muigizaji mwenzake Blandina Chagula ‘Johari’ na yeye ndio alikuwa chachu ya kuingia kwenye uigizaji.

Akizungumza na Over Ze Weekend hivi karibuni, Duma alisema kuwa hata akiulizwa mahali popote kuhusu msanii aliyemfanya aingie kwenye uigizaji hawezi kuona aibu kusema ni Johari kwa sababu mpaka leo hii ndio msanii wa kike anayempenda sana.

“Siwezi kuwa mnafiki hata kidogo ukweli ni kwamba Johari ndiye aliyenifanya niingie kwenye tasnia ya filamu kwa sababu alikuwa akiigiza kiuhalisia kwenye filamu yake ya Johari na mpaka leo ni mwanamke wa kwanza kumpenda Bongo Muvi,” alisema Duma.

NEEMA ADRIAN

Comments are closed.