The House of Favourite Newspapers

Mshindi pikipiki ‘Live’ Global TV Kesho Saa 10 Jioni

KAMPUNI ya Global Publishers haina shaka hata kidogo katika promosheni ambazo wanaziendesha ambapo habari tamu kwa wasomaji wake wa magazeti ni kwamba maisha ya Mtanzania mmoja kesho Jumanne yatabadilika kwa kujinyakulia pikipiki mpya kabisa.

Global ambayo nyuma imeshatoa zawadi ya nyumba kwa wasomaji wake, kesho Jumanne itaanza kugawa pikipiki hiyo ikiwa ni ya promosheni yake ya sasa ya Tusua Maisha na Global ambayo ina wiki mbili tangu kuzinduliwa kwake.

Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho amesema kwamba huu ni muda wa wasomaji kuanza kuvuna zawadi mbalimbali kupitia promosheni hiyo ya Tusua na Global ambapo kwa kuanza wanaanza na kutoa pikipiki mpya ambayo itatolewa kesho Jumanne.

“Tunaanza kwa kutoa pikipiki kwa msomaji wetu wa kwanza, Jumanne (kesho) msomaji mmoja atapata zawadi hiyo tena zoezi zima litakuwa mubashara kwenye Runinga ya Mtandaoni ya Global Tv Online saa 10 jioni.

“Hiyo itakuwa pikipiki ya kwanza kati ya 12 ambazo zipo, wanachotakiwa kukifanya wasomaji ni kununua zaidi tu magazeti pendwa ya kampuni yetu na kujiweka karibu zaidi na kushinda zawadi mbalimbali ambazo zipo.

“Tutakuwa tunatoa pikipiki kwa kila wiki na tumeamua kufanya hivyo kwa sababu tunarudisha fadhila kwa wasomaji wetu. Katika zawadi hizo hatutaacha hata sehemu ya jamii kwani kwa vijana kuna headphone za Beats By Dre huku kwa upande wa akina mama kutakuwa na vyombo vya nyumbani lakini pia tutatoa jezi za timu ambazo zinashiriki Kombe la Dunia tena mshindi ndiye atachagua ni jezi gani ambayo anaitaka,” alisema Mrisho.

Kushiriki promosheni hii, msomaji atatakiwa kununua magazeti ya Championi, Amani, Ijumaa Wikienda, Spoti Xtra, Ijumaa, Uwazi na Risasi Mchanganyiko kisha ajaze kuponi iliyopo ukurasa wa pili na kuituma.

 

 

 

 

 

 

Comments are closed.