The House of Favourite Newspapers

Dume Suruali Kaa Mbali Namii!-4

Studio shot of young couple smiling and looking at each otherDUME SURUALI KAA MBALI NAMII!-4

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale mama Careen alipomsikia binti yake huyo akimkaribisha mgeni ndani, akiwa na shauku ya kujua mgeni huyo alikuwa nani akamuona mpenzi wake mwingine aitwaye Michael a.k.a Meco ambaye alikuwa na fedha balaa, kwa furaha akainuka na kwenda kumkumbatia na kuanza kumvurumushia mabusu huku Careen akishuhudia. Je, kilifuatia nini? Pata uhondo…

Careen aliposhuhudia tukio hilo, aligeuka na kuelekea chumbani kwake ambapo alimwambia Cathe aende fasta sebuleni akajionee sinema.

“Sinema inahusu nini?” Cathe aliyedhani pacha wake alimanaanisha muvi iliyokuwa ikioneshwa kwenye runinga akamwuliza.

“Siyo muvi ya kwenye runinga, nenda kamwangalie mama yako anavyofanya na mgeni wake,” Careen akwamwambia.

“Anafanya nini?” Cathe akamwuliza.

Kufuatia kuuliza hivyo, Careen akasisitiza aende fasta akajionee na apunguze maswali.

Kama alivyofanya awali, msichana huyo alitembea kwa kunyata hadi mwisho wa korido akajibanza na kuchungulia kwa tahadhari, akamuona mama yake ambaye kanga aliyojifunga ilianguka chini akiwa amekumbatiana na Meco huku midomo yao imenatiana.

Kwa kuwa Meco na mama yake walizama kwenye mahaba mazito, walifumba macho hivyo kushindwa kumuona Cathe aliyezubaa kwa sekunde kadhaa akiwa kawatumbulia macho kisha alichomoka mbio na kwenda chumbani kwao.

“Careen hivi huyu mama ana nini?” Cathe akamwuliza pacha wake.

“Hata mimi nimejiuliza bila kupata jibu,” Careen alimjibu.

“Yaani ashakumu si matusi, mama amekuwa malaya wa kupitiliza, hivi si punde tu alikuwa na mwanaume mwingine?” Cathe akamwuliza nduguye.

“Sasa Careen, unaniulizaje wakati wewe mwenyewe ulimuona baba yetu handsome?” Cathe akamwambia.

Careen alimjibu Cathe kwamba alimuona na kumsikitikia mama yao na kujiuliza kwa nini alikuwa akifanya mambo yale ya chumbani zaidi bila kujali kama walikuwepo pale nyumbani.

“Mimi naona tukae na mama kisha tuzungumze naye, kama atachukia au kutufukuza hapa nyumbani poa tu ila lazima tumwambie anavyofanya siyo vizuri,” Careen alimwambia ndugu yake.

“Itakuwa poa, mama anapaswa kujua sisi tumekua wakubwa sasa, kufanya hivyo mbele yetu siyo vizuri,” Cathe akamwambia nduguye.

Ingawa wasichana hao walikerwa na tabia ya mama yao, Careen alimwambia mwenzake ngoja akajionee tena sinema ya bure, akatoka chumbani kwao kwa kunyata na kuelekea sebuleni.

Alipofika mwisho wa korido alipotupa macho sebuleni, alichokiona kilimduwaza na kumfanya mwili kumsisimka, mama yake na Meco walikuwa wakifanya mapenzi juu ya sofa la watu watatu, akatoka mbio kwenda chumbani kwao.

“Kuliko mwenzangu mbona umerudi mbio?” Cathe akamwuliza pacha wake.

Careen alipoulizwa hivyo, kwa sauti ndogo akamwambia Cathe aende akajionee kilichomfanya arudi mbio.

Kama nilivyokwambia kwamba, mapacha hao walikuwa watundu sana, Cathe alipoambiwa hivyo bila ya woga alinyata na kwenda kujionea sinema ya bure.

Kama ilivyokuwa kwa mwenzake, aliweza kuwaona laivu mama na mpenzi wake Meco wakiwa kwenye mechi kali ya kukamiana, huku mzazi wao aliyenogewa akiangua kilio cha mahaba.

Kwa kuwa tayari alipevuka, mwili ulimsisimka si kidogo akatoka mbio na kurudi chumbani kwao akaketi kitandani na kumwangalia pacha wake bila kusema chochote.

“Umejionea hiyo sinema?” Careen alimwuliza pacha wake.

“We acha tu!” Cathe akamjibu.

“Umeona mambo ya mama yako?” Careen akazidi kumwuliza mwenzake.

Cathe alimwambia aliyaona na kwamba mwili wote ulimsisimka na kutamani kuwa na mpenzi ili naye afurahie dunia kama ambavyo mama yao alikuwa akifanya na wanaume tofauti.

“Hata mimi nilitaka kukwambia hivyo hivyo, lakini ukiacha hiyo raha inatupasa tujue kuna faida gani nyingine kubwa ya mambo hayo!” Careen alimwambia Cathe.

“Ila ni kweli, tusije tukajiingiza kwenye mambo hayo halafu tukafa kwa Ukimwi na kutofikia malengo yetu ya maisha,” Cathe alimwambia mwenzake.

Wakati mapacha hao wakiendelea na mazungumzo, wakasikia watu wakizungumza kisha wakasikia mlango wa kuingilia chumbani kwa mama yao ukifunguliwa.

Baada ya dakika tano Careen alitoka kwa kunyata ili akachungulie sebuleni, alipoufikia mlango wa chumba cha mama yao alisikia kitanda kilivyokuwa kikilamika huku mama yao akiangua kilio kilichokwenda sambamba na kumsifia Meco alivyokuwa akimpa raha!

Msichana huyo akawa katika wakati mgumu sana, alichokifanya ni kurudi chumbani kwao akamwambia Cathe ambaye naye alikwenda pale mlangoni kusikiliza kilichokuwa kikijiri.

“Careen, umeona baba zetu wanavyomliza mama? Yule wa kwanza mambo aliyaweza, huyu naye usipime, si umemsikia mama yako anavyolia na kutokwa na maneno mfululizo?” Cathe alimwambia mwenzake.

Kufuatia kauli hiyo ya Cathe, Careen alicheka na kumwambia alishuhudia kila kitu na kumfahamisha mwenzake huyo kwamba jinsi jamaa huyo alivyokuwa na mwili mkubwa wa mazoezi mama yao alikuwa na haki ya kulia na kutokwa na maneno mfululizo ya kimahaba.

“Unajua mimi sijamuona vizuri, hivi ana mwili mkubwa eh?” Cathe alimwuliza pacha wake.

“Kajazia na ana kifua kipana kama cha yule baunsa Livingstone,” Careen akamwambia.

Wakati mapacha hao wakizungumza, mara mlango wa chumbani kwao ukafunguliwa na mama yao aliyejifunga kanga akaingia.

Je, kilifuatia nini? Usikose uhondo huu wiki ijayo.

Comments are closed.