The House of Favourite Newspapers

Umri mzuri wa kuzaa kwa mwanamke-2

couple-with-a-baby-4Ilipoishia wiki iliyopita.

Kwa kulinganisha kati ya kundi la umri wa miaka 25-29 na 30-34, wanawake wa miaka 30-34 wenye mimba za kwanza walikuwa na hatari ya kuzaa watoto njiti kwenye wiki 22-31 za ujauzito au kuzaa watoto wafu. Endelea na makala haya…

couple-with-a-baby-2Kikosi cha watafiti kiligundua pia sababu zingine zinazoweza kuleta matatizo ya uzazi mfano wa sababu hizo ni kama kuvuta sigara au kuwa mnene kuliko kawaida.

KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI (MENOPAUSE)

Wanawake wengi huanza kipindi cha kukosa hedhi wakiwa na umri wa miaka 40 na kuendelea lakini kwa wengine huanza wakiwa wamechelewa wakiwa na miaka 60. Kutokana na mabadiliko ya kiwango cha homoni kinachotokeza, huenda mwanamke akakosa kupata hedhi mapema wakati ambao hakutarajia au akavuja damu nyingi isivyo kawaida wakati wa hedhi.

couple-with-a-baby-3Kipindi cha kukoma hedhi huwa tofauti kwa kila mwanamke. Dalili zinaweza kuonekana kipindi hicho ni pamoja na joto la ghafla mwilini, ambalo huenda likafuatiwa na kuhisi baridi. Dalili hizo zinaweza kumfanya mtu akose usingizi na kuishiwa na nguvu.

Wengine hupatwa na hali hiyo kwa miaka mingi na wachache sana husema kwamba wao hupatwa na joto la ghafla mara kwa mara maisha yao yote.

couple-with-a-baby-1Ni busara mtu afanyiwe uchunguzi wa kiafya kabla ya kuamua kwamba joto la ghafla linasababishwa na kukoma kwa hedhi. Kwa kuwa kuna matatizo mengine ya kiafya yanaweza kuleta joto la ghafla mfano ugonjwa wa malaria, homa ya matumbo n.k.

Mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kupunguza baadhi ya matatizo hayo mfano kuacha kuvuta sigara, kupunguza au hata kuacha kunywa pombe, vinywaji vyenye kafeini na vyakula vyenye sukari au vikolezo ambavyo vinaweza kusababisha joto la ghafla mwilini.

Kufanya mazoezi husaidia sana kupunguza matatizo yanayohusishwa na kukoma kwa hedhi. Kwa mfano, mazoezi yanaweza kupunguza kukosa usingizi na kusaidia kuboresha hali ya kihisia na pia huimarisha mifupa na afya ya mwanamke.

Ili kumsaidia mwanamke kukabiliana vizuri na kipindi hicho cha kukoma kwa hedhi, huenda madaktari wakampa homoni, vitamini na madini, na dawa za kutibu kushuka moyo.

Pia ni jambo la busara kuwaambia uwapendao hali unayoikabili ili wakuonyeshe upendo na wakupe msaada unaouhitaji wakati wa hali yako. Kipindi hicho kinapokwisha, wanawake ambao hutunza afya yao, wanapata tena nguvu na kuendelea kufurahia maisha.

Comments are closed.