The House of Favourite Newspapers

Ebitoke na Skendo ya Kujichubua

BAADA ya habari kuzagaa kwamba kwa sasa anatumia mkorogo (anajichubua) ndiyo maana amekuwa mweupe ghafla, mchekeshaji maarufu Bongo, Anastazia Exavery ‘Ebitoke’ ameibuka na kukanusha vikali skendo hiyo.

 

Akichonga na Risasi Jumamosi, Ebitoke alisema weupe wake umetokana na joto kuwa kali na katika vitu ambavyo hawezi kuvifanya ni kujichubua kwa sababu anaelewa wazi kuwa kuna madhara makubwa endapo atafanya hivyo.

 

“Najua madhara ya kujichubua siwezi kufanya hivyo kama watu wanavyonituhumu, nimebadilika na kuwa mweupe siku hizi tofauti na zamani kwa sababu ya joto tu na siyo vinginevyo,” alisema Ebitoke.

Stori: Memorise Richard, Dar.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.