The House of Favourite Newspapers

EFM Yanyakua Tuzo 4 kwa Mpigo

efm-tuzo-1

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Efm, Dennis Ssebo akipokea tuzo kwa niaba ya Efm.

EFM redio imejinyakulia tuzo NNE usiku wa kuamkia leo katika Tuzo za Tanzania Leadership Awards (T.L.A- 2016) kwa vipengele vya Redio Bora ya Mwaka, Kampuni Bora kwa Ubunifu, Kampuni Inayokua kwa Kasi pamoja na Tuzo ya Mwandishi Bora wa Mwaka ambayo imekwenda kwa mtangazaji wa Kipindi cha Uhondo katika redio hiyo, Dina Marios.

Hafla ya ugawaji tuzo hizo ilifanyika jana, 27/1/2017 katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel, Posta jijini Dar.

efm-tuzo-2

Wafanyakazi wa Efm wakiwa katika picha ya pamoja na tuzo zao.

Ni mwaka wa pili mfululizo kwa redio hiyo kuchukua Tuzo za Tanzania Leadership Awards ambapo tuzo ya kwanza waliipata mwaka jana kwa kipengele cha Redio Bora ya Mwaka.

Ikiwa ni  takribani miaka mitatu tangu redio hii ianzishwe,  imejipatia umaarufu mkubwa kwa kuutangaza Muziki wa Singeli na kujihusisha na mambo mbalimbali ya kijamii kupitia matamasha, vipindi na kampeni mbalimbali kama vile kupanda miti (mti wangu), kuanzisha vikundi vya mazoezi (Efm Jogging Club), kampeni za afya, kuhamasisha jamii kujikita katika shughuli za ujasiriamali, pia kutatua matatizo katika jamii  kwa lengo la kujiweka karibu na jamii nzima.

Comments are closed.