The House of Favourite Newspapers

Hivyo ndivyo wauza mihogo barabarani wanavyojiuza!

mihogo-3 

WAANDISHI WETU | RISASI, Dar es Salaam

KUFUATIA madai kuwa, baadhi ya wasichana wanaofanya biashara ya kuuza mihogo, karanga na nazi kwenye foleni za magari na mitaani jijini Dar, wanajihusisha na biashara ya kujiuza, Kikosi cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) kiliingia kazini na hiki ndicho kilichobainika.

MADAI YA AWALI

Baadhi ya mashuhuda walioongea na Risasi Jumamosi awali walidai kuwa, akina dada hao wawapo kwenye biashara hiyo, ukiwataka pia kwa huduma ya ngono wamekuwa ni wepesi kukubali kutokana na hali ngumu kimaisha. “Hawa akina dada unaowaona wanauza mihogo kwenye mabeseni wanapiga madili pia ya kujiuza, ukiwa kwenye gari au mtaani kisha ukamtaka unaweza kuondoka naye au anakupa namba yake kisha baadaye unamtafuta, mnamalizana,” alidai kijana mmoja anayefanya kazi ya umachinga kwenye mataa ya Ubungo jijini Dar.

mihogo-1Kamanada wa OFM na muuza mihogo.

OFM KAZINI

Kufuatia madai hayo kushika kasi, Kamanda wa OFM akiwa ndani ya gari lake maeneo ya Stendi ya Mawasiliano kuelekea Ubungo, alikutana na dada mmoja aliyejaaliwa shepu bomba akiwa anauza mihogo na mazungumzo yakawa hivi:

OFM: Shilingi ngapi mhogo?

Mdada: Kipande au mzima?

OFM: Kipande tu. Mdada: Kuna kipande cha 200, 500 na 1,000. Karanga na nazi pia zipo, si unajua tena! OFM: Nipe kipande cha mia tano na karanga lakini pia nakutaka na wewe, unasemaje?

Mdada: Aka! Sasa hivi niko kazini.

OFM: Basi nipe namba yako, nitakutafuta baadaye. Mdada huyo muuza mihogo huku akijichekesha akataja namba yake, OFM akaisevu.

MUUZA MIHOGO WA PILI

Siku nyingine kamanda wa OFM akiwa kwenye mizunguko yake maeneo ya Sinza-Mapambano jijini Dar alikutana na mdada mwingine muuza mihogo na mazungumzo yakawa hivi:

OFM: (Huku akionekana kum changamkia kana kwamba wanajuana) nataka kipande kidogo cha nazi na muhogo pamoja na wewe mwenyewe, unasemaje?

Mdada: Mh! Wewe ule kwanza mihogo na karanga zako kisha unitafute baadaye.

OFM: Baadaye tutaonana vipi sasa?

Mdada: Simu yangu imezima chaji, niachie namba yako basi halafu nitakutafuta. OFM akamuachia namba kisha wakaagana. Saa 2.30 usiku Katika kutaka kuthibitisha kama kweli akinadada hao wanafanya biashara hiyo ya kujiuza, ilipofika saa 2.30 usiku, kamanda wa OFM alimpigia simu yule dada wa kwanza, mazungumzo yakawa hivi;

OFM: Mambo?

 Mdada: Poa, nani?

OFM: Najua huna namba yangu, mimi tulikutana pale Ubungo mataa, ukanipa namba yako.

Mdada: Aaa! Nimekukumbuka, niambie, nakusikiliza.

OFM: Ni hivi, mimi nimevutiwa na wewe, nakutaka kimapenzi, nikuandalie shilingi ngapi?

Mdada: Mh! kwani uko wapi?

OFM: Hapa Mwenge. Vipi unaweza kuja?

Mdada: Saa hizi itakuwa ngumu maana naishi mbali, tufanye kesho. Mwingine aingia mzimamzima Katika utafiti huo, OFM ilifanikiwa kukutana na dada mmoja anayeuza mihogo maeneo ya Buguruni Chama na alipotakiwa kutoa huduma ya ngono aliweka wazi kuwa, kama ni kulala aandaliwe 20,000 lakini kwa ‘short time’ ni 5,000!

Kutoka Risasi Jumamosi

Kufuatia uchunguzi huo uliobaini ni kweli kwamba baadhi ya wasichana wanaouza mihogo mtaani na kwenye barabara wanajiuza, tunawashauri wanaofanya hivyo kuacha kwani wanajihatarishia maisha yao. Wanaokubali kuchukuliwa na wanaume ambao hawawajui kwa lengo la kwenda kufanya nao ngono kwanza ni hatari kwa afya zao lakini huenda wanaume hao wana malengo yao mengine mabaya!

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.