The House of Favourite Newspapers

Efm Yawakutanisha Wanawake Wajasiriamali

0

1Mgeni rasmi Devotha Likokola akiongea na wanawake wa vikundi mbalimbali kuwapa (hawapo pichani).
2Mmoja wa wajasiriamali Ester Dalali akitoa ushuhuda kuhusu maisha yake.
3Msemaji wa Kampuni ya Graca Machel akizungumza na wanawake (hawapo pichani)
4Wanawake wa vikundi mbalimbali wakibadilishana mawazo na mgeni rasmi.
6Likokola akikata keki.
7Baadhi ya wanawake kutoka vikundi mbalimbali wakilishwa keki na Mh. Devotha Likokol.
10Likokola akipokea tuzo  ya mwanamke wa shoka kutoka kwa mtangazaji wa Efm radio katika kipindi cha uhondo, Dina Marios.12Muda wa maakuli ukafika.13Akina mama wakiserebuka na muziki wa taarab kutoka Jahaz Modern Taarab. 

Katika kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Kituo cha Redio cha EFM kilichopo Kawe jijini Dar, jana kimevikutanisha vikundi mbalimbali vya ujasiliamali na VICOBA kutoka mkoa wa Pwani na jiji la Dar es Salaam.

Tafrija hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Litostar Park uliopo maeneo ya Salasala jijini humo ikiwa na lengo la kuwapa wanawake elimu ya ujasiliamali, kujitambua pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika biashara na maisha kwa ujumla.

Aidha mgeni rasmi katika tafrija hiyo alikuwa Raisi wa VICOBA nchini, Devotha Likokola ambaye amewataka wanawake nchini kuwa wajasiriamali na wenye kuthubutu kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Leave A Reply