The House of Favourite Newspapers

Eric Shigongo Awapongeza Wahitimu IFM, Awasihi Wasibwete!

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo jana aliwapongeza watoto wake kwa kuhitimu masomo yao katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kilichopo Posta jijini Dar.

01Wahitimu, kulia ni Anna Mabula akiwa na Kulwa Deogratias  kwenye pozi.

1Wahitimu Anna, Kulwa na Dorice wakikata keki kwenye tafrija yao.

2 3 4

Wahitimu wakilishana keki

5

Anna akimlisha keki mjomba wake Shigongo.

6 7

Wanafamilia wakiwa kwenye maombi.

8 9 10

Mke wa Shigongo, Mama Vene Shigongo Jackline wa kitoa zawadi kwa wahitimu.

11 12 13

Picha mbalimbali za wanafamilia.

14

Kaka wa wahitumi, James Bukumbi akitoa nasaha kwa wadogo zake (hawapo pichani)

15

Mwana muziki Moses akitumbuiza na wanabendi wenzake.

moses-akiwa-na-wahitimu shigongo-akiwa-na-wanamuziki-wa-bendi-ya-moses-aliokuwa-wanatumbuizaShigongo akiwa na Bendi ya Moses.

Wanafunzi hao ambao wamehitimu Shahada ya Uhasibu na kutunukiwa vyeti katika Uwanja wa Karimjee jijini Dar, na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ni Kulwa Deogratius, Anna Mabula na rafiki yao kipenzi Dorice.

Hafla fupi ya kuwapongeza wahitimu hao ilifanyika nyumbani kwao Mikocheni, Dar jana na kuhudhuliwa na baadhi ya ndugu, marafiki pamoja huku bendi iliyokuwa ikitumbuiza, ikiongozwa na mtaalamu wa kupiga saxophone (mdomo wa bata), Moses.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Shigongo aliwaasa wahitimu hao kutokubweteka na elimu waliyoipata kwani maisha ni mapambano na wanapaswa kupambana zaidi ikiwemo kuongeza elimu ili kulisaidia taifa.

“Nina furaha sana kuwaona mkiwa mmehitimu salama, nafahamu kulikuwa na ugumu, makwazo na mambo mengine mengi lakini Mungu amewasaidia mmehitimu vyema.

“Basi msibweteke kwani maisha ni mapambano, ikiwezekana muongeze elimu zaidi na zaidi ili siku moja muwe viongozi wakubwa wa nchi na dunia kwa ujumla,” alisema Shigongo.

Na mwandishi wetu

Comments are closed.