The House of Favourite Newspapers

Esha Asimulia Alivyotaka Kujiua na Mwanaye!

Esha na mwanaye.

UKITAJA listi ya wasanii wanaofanya vizuri kwenye filamu Bongo, huwezi kuacha kulitaja jina la Esha Buhet ambaye alianza kun’gara kwa mara ya kwanza kwenye filamu ya Mrembo Kikojozi.

Msanii huyu japo amejulikana zaidi kupitia kazi yake ya filamu lakini pia amejiongeza kwa kufanya kazi nyingine ikiwemo ya mama nt’ilie na hapa chini amefanya mahojiano na gazeti hili na kuzungumza mengi kuhusiana na kazi zake na maisha kwa ujumla.

 

Showbiz Xtra: Kwanza wasomaji wangependa kujua bado unaendelea na mambo ya usanii au umekacha?

Esha: Hapana sijaachana na mambo ya usanii lakini kwa sababu nilikuwa nimejifungua ndiyo maana nimekuwa kimya.

Showbiz Xtra: Watu wengi wanajua umeukacha uigizaji badala yake umeingia kwenye mambo ya mama nt’ilie kuna ukweli wowote?

 

Esha: Hapana niliona wakati huu nimejifungua na siwezi kufanya kazi za sanaa hivi karibuni nikaamua kujiongeza kufungua kimgahawa hapa nyumbani kwa-ngu.

Showbiz Xtra: Ulijifunzia wapi mambo ya kupika maana watu wengi siku hizi wanakujua maarufu kwa kupika vitumbua.

Esha: Mimi nilifundishwa na marehemu mama yangu kupika kila kitu na nilijua wazi ndiyo hazina yangu ya pili kwenye maisha na siyo kukalia kitu kimoja.

Showbiz Xtra: Mastaa wengi wanapenda kucha zao na kujiremba wewe umewezaje kukubali kukaa jikoni muda wote kuungua na moto?

 

Esha: Sasa maisha siyo muda wa kujiremba na kufuga kucha wanaofanya hivyo wanachelewa sana.

Showbiz Xtra: Ulishawahi kuumizwa na kitu gani maishani na kukukosesha amani?

Esha: Niliumizwa sana na mapenzi, yakanitesa mno mpaka nilifikia hatua ya kutaka kunywa sumu na nimnyweshe mwanangu tufe.

Showbiz Xtra: Kwa sababu gani na uliumizwa na nani kiasi cha kutaka kunywa sumu?

 

Esha: Nisingependa kumtaja ila nashukuru sasa mambo ni mazuri na maisha yanaendelea kama kawaida.

Showbiz Xtra: Nini kilikufanya ukarudisha furaha yako tena na kuwa sawa kama zamani?

Esha: Nilipopata ujauzito wa mtoto wangu wa pili kila kitu kilibadilika kwa kweli na furaha yangu ikarudi.

Showbiz Xtra: Katika biashara yako hii ya kupika mastaa wenzako wanakuunga mkono?

Esha: Ni baadhi maana sisi kwa sisi mara nyingi kuungishana ni tatizo na sijajua kwa nini.

 

Shobiz Xtra: Kwa nini umeamua kufanya hii biashara ya chakula nyumbani kwako badala ya sehemu nyingine.

Esha: Kwa sababu bado nina mtoto mdogo sana hivyo nikiwa hapahapa mazingira ya nyumbani ni afadhali.

Showbiz Xtra: Vipi mume wako anakuunga mkono katika biashara yako?

 

Esha: Tena mwanzo mimi nilikuwa nataka mambo ya saluni yeye akaniambia mke wangu si unajua kupika fanya biashara hiyo.

Showbiz Xtra: Ulishawahi kulala nje kwenye maisha yako kwa kukosa pa kulala?

Esha: Mara nyingi sana siyo mara moja na hiyo ni baada ya mama yangu kufariki maana nilikuwa mimi na yeye tu.

Showbiz Xtra: Nakushukuru sana Esha kwa ushirikiano wako.

Esha: Karibu sana.

 

IMELDA MTEMA | GAZETI LA AMANI

Kwa habari zingine kama hizi, utazipata kupitia Application ya Global Publishers.

Comments are closed.