The House of Favourite Newspapers

Esha: Uzazi Umenifanya Niwe Mjasiriamali

0

 

STAA wa filamu za Kibongo, Esha Buheti amedai kuwa baada ya kuongeza familia kwa kumpata mtoto mwingine amejikuta amekuwa mjasiliamali moja kwa moja kwani bila kufanya hivyo vyuma vitazidi kukaza.

 

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Esha alisema kuwa kwa sasa amekuwa mjasiliamali kwani ana uwezo wa kupika chakula cha shughuli mbalimbali, keki na mbali na mapishi pia anao uwezo wa kupamba wanawake wenzake kwa kuwapaka Make up vitu ambavyo hakuvifanya kabla kwani alikuwa akiigiza tu na kupika siku mojamoja alipokuwa akipenda.

 

“Uzazi umeninyoosha acha tu bila kujituma kwa kufanya kazi mbalimbali vyuma vitakaza na itakula kwangu pamoja ya kuwa baba yupo lakini mimi kama mama lazima nichape kazi pia,” alisema Esha.

STORI: HAMIDA HASSAN

Leave A Reply