The House of Favourite Newspapers

Esma Aanika Siri Kuikacha Pati ya Zari

Esma Platnumz.

ZARINAH Hassan ‘Zari’ na wifi yake Esma Abdulkadir ‘Esma Platnumz’ wamedaiwa kuwa kwenye bifu zito ndani ya kipindi chote cha mwaka 2017 ambapo kitendo cha Esma kuikacha pati ya mtoto wa Zari, Nillan iliyofanyika juzikati kule Sauzi kinatajwa kuchangiwa na kutoiva kwa wawili hao, Risasi Jumamosi linakupakulia hii kinagaubaga.

 

Kikilimwagia ubuyu gazeti hili, chanzo kilicho karibu na wawili hao kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, tangu kipindi kile Esma amshike Mobeto hadi kufikia hatua ya kuzaa na kaka yake, Zari amekuwa akimchukia na ndiyo sababu kubwa ya kutoiva kwao.

 

“Esma na Zari bado hawako vizuri kabisa, yaani ule ushosti wa Esma na Mobeto ndiyo chanzo, ukimuuliza Esma atakwambia yuko vizuri na Zari lakini ukweli hawako poa na ndio maana ile pati ya juzi kule Sauzi wameenda ndugu karibia wote lakini Esma aliikacha,” kilidai chanzo hicho.

Mrembo Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Baada ya ubuyu huo kumwagwa kwenye meza ya gazeti hili, hatua iliyofuata ni kumtafuta Esma ili kufungukia madai hayo, ambapo alipopatikana alisema anajua wengi wataongea wanavyojua kuhusu yeye kutoenda kwenye pati hiyo, lakini ukweli ni kwamba, biashara yake mpya ya duka aliyofungua ndio sababu.

 

“Nisingeweza kuiacha biashara yangu ya duka ambalo nimelifungua hivi karibuni alafu niende kwenye pati, wateja wangu wasingenielewa kabisa na ningerudi ingenichukua muda kuwarejesha. “Watu wanapenda kuongea sana, mimi na Zari wala hatuna tatizo lolote, kama hamuamini siku nyingine akiandaa pati nitaenda tu,” alisema Esma.

STORI NA IMELDA MTEMA

Comments are closed.