The House of Favourite Newspapers

Ethiopia Yafukuza Maafisa 7 Umoja wa Mataifa

0

MAAFISA saba wa Umoja wa Mataifa wamepewa muda wa saa 72 kuondoka Ethiopia kwa kile ambacho serikali ya nchi hiyo imedai kujiingiza katika mambo ya ndani ya Ehtiopia, wakati huo huo shinikizo linaongezeka dhidi ya serikali ya Ethiopia kuhusu jimbo la Tigray.

 

Serikali ya Ethiopia imechukua uamuzi wa kuwafukuza maafisa hao wa Umoja wa Mataifa baada ya wafanyakazi wa kutoa misaada kusababisha juu ya hali ya maafa katika jimbo la Tigray inayotokana na kushindikana kupeleka misaada kwenye sehemu hiyo.

 

Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imesema wafanyakazi saba wa mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa wanatakiwa kuondoka nchini Ethiopia, ikiwa pamoja na naibu mratibu wa misaada nchini humo Grant Leaty na mwakilishi wa shirika la watoto la UNICEF, Adele Khodr.

 

Leave A Reply