The House of Favourite Newspapers

ETI HARMORAPA HAJAISHIWA KIKI!!!

UNAMKUMBUKA Kiboko ya Mabishoo Harmorapa? Basi ameibuka na kuiambia Showbiz kuwa, eti bado hajaishiwa kiki mjini bali zinaendelea kumfuata zenyewe.

 

Harmorapa ambaye jina lake halisi ni Athuman Omary alisema kuwa, japokuwa hajitokezi hadharani, lakini inapotokea kitu ‘kime-trend’ anazungumziwa sana kwenye mitandao hivyo huwezi kusema ameishiwa kiki.

 

“Kiki kwangu zinanifuata zenyewe! Mitandao bado inanifanya niendelee kukiki kwa sababu inapotokea jambo la kuchekesha, lazima watanitaja tu,” alisema Harmorapa ambaye kwa sasa amekuja na projekti mpya akiwa na Mkali Wenu iitwayo Valentine’s Boy.

Na Andrew Carlos | Ijumaa

Comments are closed.