The House of Favourite Newspapers

ETO’O : KUMCHUKUA MTOTO WA DOKII!

Samuel Eto’o na Ummy Wenceslaus ‘Dokii’

MCHEZAJI wa Cameroon, Samuel Eto’o amekubali kumchukua mtoto wa muigizaji Ummy Wenceslaus ‘Dokii’, Wenceslaus Halfan kwenda kumtafutia soko la mpira nchini mwao.

Akizungumzia ishu hiyo, Dokii alisema hivi karibuni alikutana na Eto’s katika Hoteli ya Ramada, Mbezi Beach jijini Dar na katika mazungumzo, alimweleza kuhusu mwanaye huyo anayecheza Singida United ya watoto na ndipo alipoonesha kumsaidia.

“Alikubali kumchukua, alisema atakwenda kumfanyia mipango na kisha tutawasiliana. Ameguswa na mimi single mother, ameahidi kunisaidia,” alisema Dokii.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.