The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE: Sapraizi ya AY na King Kikii ni Habari Nyingine – Video

BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, nguli wa Bongo Fleva, Ambwene Allen Yessayah ‘AY’,  amesema tayari ameshaandaa video ya wimbo wake mpya ambao amemshirikisha mkongwe wa muziki nchini, Mzee King Kikii na video hiyo ataiachia rasmi Novemba 28, mwaka huu.

Hit-Maker huyo wa ngoma ya ZIGO amesema wimbo wake huyo mpya unaitwa SAFARI ambao unaelimisha, unaliwaza na kuburudissha lakini pia unaweza kusikilizwa na mtu yeyote bila kujali rika.

Rapa huyo ameongeza kuwa ukimya wake kwenye game si kwamba anakuwa hafanyi muziki,  bali anafanya sana tu lakini anajipa muda kuangalia ni muziki wa aina gani unahitajika sokoni na namna ya kwenda navyo sawa vitu hivyo.

“Collaboration yangu mimi na mzee King Kikii, intokana na kumsikia kwenye moja ya interview zake akisema anatamani kufanya kazi na mimi. Ilinipa moyo sana nikamtafuta tukafanya collaboration.  Ninaamini ni kazi ambayo itakaa na kudumu kwenye industry kwa muda mrefu,” alisema AY.

 

EXCLUSIVE: AY Afunguka “Sio Diamond tu, Hata mimi Nilishafungiwa”

Comments are closed.