The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE VIDEO: MREMA AIBUKA, AWAFUNGUKIA KINANA NA MAKAMBA

Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP),  Augustino Lyatonga Mrema akifanya mahojiano na Catheline Kahabi (kushoto) wa Global TV Online.

 

ALIYEKUWA Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa TLP,  Augustino Lyatonga Mrema,  amefanya mahojiano na Global TV Online na kusea wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatakiwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa juhudi anazozifanya kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

 

Ameongelea waraka wa makatibu wastaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, akisema watu hao walitakiwa kulifanya jambo hilo kimyakimya bila watu wengine  kujua  kuliko kulitoa hadharani kwenye magazeti na mitandao  na kwamba ingewabidi hata kwenda mahakamani kumshitaki Cyprian Musiba.

 

Aidha, amesema ndani ya CCM  hakuna mgogoro,  akaongeza kwamba mwenyekiti wake, Dkt. John Magufuli,  ni mtu makini na muhimu kwa nchi yetu na wao kama TLP wameshampitisha kuwa mgombea wao katika uchaguzi ujao na watamuunga mkono.

Comments are closed.