FAHAMU MAKUNDI YA UGONJWA WA PUMU (BRONCHIAL ASTHMA)-2

Wiki hii tunaendelea mfululizo wa makala ya Fahamu makundi ya ugonjwa wa pumu, endelea kufuatilia…

LAKINI pia upasuaji wakati wa kujifungua (Caesarian section), tafiti kadhaa zimeonesha kuwa kujifungua kwa njia ya upasuaji huongeza uwezekano wa kupata pumu kwa vile njia hiyo yaweza kuathiri mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya maradhi.

MAKUNDI YA PUMU

Pumu inaweza kugawanywa katika makundi mawili;

PUMU YA GHAFLA (ACUTE ASTHMA)

Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali ya kawaida katika njia zao za hewa isiyobadilika kati ya shambulizi moja na jingine.

PUMU SUGU (CHRONIC ASTHMA)

Kundi hili la pumu huwa na tabia ya kuwa na njia nyembamba za kupitisha hewa na kadiri jinsi mgonjwa anavyoendelea kupata matukio zaidi ya pumu, njia za hewa huzidi kuwa nyembamba zaidi. Bila kujalisha mgonjwa anaingia katika kundi gani, ugonjwa wa pumu unaweza kugawanywa katika aina kuu nne; Ambazo ni;

Kuna pumu inayobadilika (Brittle Asthma); Kulingana na tabia ya kujirudiarudia kwa matukio ya ugonjwa huu na madhara yake kwa mgonjwa, aina hii ya pumu inaweza kugawanywa zaidi katika aina nyingine mbili ambazo ni; Aina ya kwanza ya pumu inayobadilika (Type 1 Brittle Asthma) ni pumu yenye tabia ya kuwa na matukio na mashambulizi ya kubadilika kila mara japokuwa mgonjwa anaweza kuwa anapata matibabu kadhaa.

Aina ya pili ya pumu inayobadilika (Type 2 Brittle Asthma) ni pumu ambayo mgonjwa anatokea kupata shambulizi la ghafla (Asthmatic Attack) wakati hapo awali ugonjwa wake uliweza kuthibitiwa kwa matibabu. Pumu hatari isiyobadilika (Status Asthmaticus): Hii ni aina ya pumu iliyo hatari zaidi kwa mgonjwa. Pamoja na matumizi ya dawa kadhaa, zikiwemo vitanua njia za hewa (bronchodilators) na vipoza mcharuko mwili (steroids), mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu haraka na anaweza kupoteza maisha.

MWISHO.


Loading...

Toa comment