The House of Favourite Newspapers

Fainali ya BSS 2015 Dar, Kesho Dar

0

Fainali za shindano hilo zinatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa Oktoba 9 Mwaka huu  katika Ukumbi wa King Solomon  uliopo eneo la Namanga Kinondoni jijini Dar es Salaam.  Siku hiyo pia kutakuwa na burudani za nguvu kutoka kwa msanii Run Town wa Nigeria ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Gallardo.

“Ukiachia mbali msanii huyo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa Christian Bella, Yamoto Bendi, Nevy Kenzo ambao watakamua sambamba na wasanii mahiri ambao ni zao la BSS kama Peter Msechu na Kala Jeremiah.  Viingilio siku hiyo vitakuwa 25,000/=, ambapo nafasi za VIP zitakuwa 50,000/= na viti maalum vitalipiwa 100,000/=.  Nawaomba mashabiki waje kwa wingi maana fainali ya mwaka huu ni ya kipekee kabisa,” alisema Madam Ritha.

Leave A Reply