The House of Favourite Newspapers

Mashabiki Wampa Gwala FAIZA kwa Kubadilika

MASHABIKI waliojitokeza kwenye Hoteli ya Serena, wamemsifia msanii wa filamu Bongo, Faiza Ally kwamba amebadilika katika suala zima la mavazi tofauti na zamani ambapo alikuwa akijiachia nusu utupu akiwa kwenye matamasha.

Mashabiki hao walimsifia juzikati katika onesho la mavazi lililoandaliwa na mwanamitindo maarufu, Ally Rehmtullah ambapo walisikika wakinong’ona kuwa msanii huyo ameamua kufuata maadili ya Kitanzania.

“Unajua nilikuwa namsuburia Faiza afike kwa kuwa najua huwa anamsapoti sana Ally, kwa hiyo nilijua atakuja na kivazi cha ajabu kama kawaida yake kuacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi, lakini safari hii naona amevaa vazi konki na amependeza kwa kweli,” alisema shabiki mmoja.

Za Motomoto lilifanikiwa kuzungumza na Faiza na kumuuliza kulikoni ameamua kubadilika kimavazi ambapo alijibu;

“Nimeamua kuvaa vazi hili kwa sababu nimeona litanipendeza na kwa sasa sihitaji kuzungumziwa mimi kila ‘red carpeti’ naonekana nimevaa nguo ambazo siyo poa kwa hiyo kwa leo naona mashabiki zangu nimewakonga nyoyo zao.”

NEEMA ADRIAN

Comments are closed.