The House of Favourite Newspapers

MAMA GODZILLA AMLIZA RAYVANNY “Mwanangu Amelala Jamani” – VIDEO

Taarifa iliyotufikia hivi punde ni kuhusiana na Tasnia ya Bongo Fleva kupata pigo baada kuondokewa na Rapa maarufu nchini, Godzilla ambaye amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo Jumatano, Februari 13, 2019 akiwa nyumbani kwao, maeneo ya Salasala, Dar es Salaam.

Majonzi yametawala nyumbani kwa msanii huyo huku Mama yake mzazi akimtoa machozi kila ambaye amefika msibani hapo na kumtazama kutokana na jinsi anavyoomboleza.

Mwanamuziki kutoka WCB, Rayvanny, amefanikiwa kufika msibani hapo na kuonana na mama huyo ambaye kwakweli anatia huruma.

Comments are closed.